Jumapili, 4 Machi 2018

DAVID DE GEA KULIPWA PESA NDEFU KULIKO GOLIKIPA YEYOTE DUNIANI

Bodi ya mashetani wekundu wa Old Trafford Manchester united wamejipanga kumtengea Mkataba mnono Golikipa wao David De Gea .De Gea aliyebakiza mwaka mmoja klabuni hapo huku Klabu ya Real Madrid ikiendelea kutajwa kumtaka kipa huyo raia wa Spain na Golikipa wa timu ya Taifa ya Spain..
Imeeleezwa Man U wako tayari kumlipa mshahara mkubwa sawa na Mchezaji mwenzie Alexis Sanchez anaelipwa mshahara mkubwa zaidi hata ya Paul Pogba na Zlatan Ibrahimovich..na Kumfanya kuweka record ya Golikipa anaelipwa Zaidi Duniani hivyo kumfanya asiwaze kutimkia Real Madrid.

Fc Barcelona Wakaribia Ubingwa

Klabu ya Fc Barcelona Jana imeitandika Atletico Madrid kwa 1-0 goli lililofungwa na Mshambuliaji Lionel Messi.
  Kufuatia ushindi huo sasa Barcelona wanamzidi Point 8 Atletico Madrid ambae yuko nafasi ya Pili katika Ligi kuu ya Spain La Liga huku Mabingwa watetezi Real Madrid wakiwa nafasi ya 4.